WASHIRIKI
UWEZESHAJI WANAWAKE KUPITIA RIADHA
Mradi wa “Uwezeshaji Wanawake kupitia Riadha” unaratibishwa na Banda la Mabingwa kwa kushirikiana na taasisi 5 kutoka Africa, Asia na Ulaya, katika kipindi cha miezi 24 tunafanya kazi kwa pamoja kuendeleza, kujaribu na kusambaza mbinu bunifu za elimu kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupitia riadha.
BANDA LA MABINGWA
BANDA LA MABINGWA (Champions Factory) ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linaloleta mabadiliko ya kijamii kupitia ubunifu wa riadha na elimu. Banda la Mabingwa lilitengenezwa katika makao makuu yaliyopo Sofia (Bulgaria), hivyo lina ofisi London (Uingereza) na Dublin (Ireland). Kupitia mbinu bunifu za elimu, Banda la Mabingwa linakusudia kupata maendeleo na kuwezesha vijana kuwa raia hai na kufikia uwezo wao kwa kiwango cha juu. Kwa kuratibisha miradi ya elimu kimataifa na kibara, Banda la Mabingwa imeshirikisha zaidi ya vijana 1600 wasiojiweza na NEETs katika kozi tofauti. Pia, huendesha miradi katika taaluma za Elimu ya watu wazima, Elimu ya juu, Elimu na mafunzo ya ufundi, Michezo na Uendeshaji baiskeli mlimani.


ASASI YA MINE VANGATI
Mine Vaganti NGO ni shirika lisilopata faida lililozaliwa Sardinia (Italia) mwaka 2009. MVNGO ina ofisi 4 zilizopo Sassari, Olbia, Uri na Tempio Pausania na ni sehemu ya mitandao 3 ya kimataifa kama MV International, ISCA na YEE. Dhamira za taasisi hii ni kuboresha miingiliano ya kitamaduni, jamii na ujasiriamali kijani, ushirikishwaji jamii kupitia michezo, elimu isiyo rasmi inayojumuisha kuwafikia wasiojiweza. MNNGO ni mtoaji elimu ya mafunzo katika ngazi ya kijamii na barani ulaya, pia ni mshauri wa vyombo binafsi na vya kiserikali katika kuboresha na kuendeleza miradi ya vijana, watu wazima, VET, HEI, Sekta za Riadha za Ulaya na za bara shirikishi.
JAMII YA NEEMA
Taasisi ya Jamii ya Neema ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyopo Nairobi – Kenya. Shughuli zake zimejikita katika kuwezesha jamii kiuchumi na kiufahamu ili kutengeneza jamii inayojitegemea, isiyo na umaskini na uhalifu. Miradi kuu inayoendeshwa na Neema ni: Elimu na Ushirikishwaji wa Jamii, Maendeleo yenye amani kupitia uwezeshaji wa vijana na wanawake, Programu za ubadilishanaji vijana katika maeneo ya Sanaa, Dansi n.k, Ukatili wa Kijinsia, Mafunzo/Maendeleo ya Kijasiriamali, Maendeleo ya Tovuti ya Taasisi ya Jamii ya Neema.


NENDA RIADHA NEPALI (GO SPORTS NEPAL)
GO Riadha Nepali ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyopo Nepali inayojihusisha na “elimu kupitia nyenzo ya riadha. Wanatumia riadha “Kucheza, Kuelimisha na Kuwawezesha vijana katika kukabiliana na mambo mbalimbali ya kijamii na kusaidia kupunguza umaskini, ugomvi na magonjwa katika jamii zisizojiweza. Wanatumia riadha kujiboresha kitabia katika maumbile,akili, hisia pamoja na tabia za vijana wengine katika jamii kupitia mtaala maalumu wa riadha. ‘Go Sports Nepal” hutoa programu kwa kujitolea tangu Novemba 2012. Pia, hufanya programu kwenye shule tofauti, vituo vya kulelea watoto yatima na kwenye jamii, ikishirikiana na Ubalozi wa Kimarekani katika kuratibisha kambi za ubadilishanaji viongozi ” Uwezeshaji wasichana’ ambapo hujumuisha mabinti 36 kutoka Nepali na Kalifonia ndani ya siku 7 za programu za ubadilishanaji.
KITUO CHA SANAA CHA MABINGWA
Kituo cha sanaa cha mabingwa cha Chamwino (CAC) kilianza kama dira ya Kedmon Mapana, ambaye ujana wake ndani ya Chamwino, Dodoma, Tanzania ulibainishwa kwa shughuli maarufu ya jamii ya uchezaji Ngoma. Ngoma, mchezo wa kuelezea tamaduni kwa kutumia mziki, ngoma, dansi na masimulizi ya hadithi ulikua ndio sehemu kuu ya maisha ya Wagogo kwa karne nyingi. Ngoma husafirisha historia, kanuni, elimu na utambulisho kutoka vizazi vya zamani kwenda vizazi vichanga, na imekua alama kuu imara kwenye maisha ya watu wagogo waliopo eneo la kati la Tanzania. Kwa kadri Africa inavyoendelea, karne za tamaduni za ngoma zinawekwa kwenye hatari. Kitu ambacho kimekua sehemu ya maisha kwa karne nyingi, sasa kinaweza kupotea milele katika kizazi kimoja. Upoteaji wa tamaduni hizi unaleta upoteaji wa alama muhimu ya utambulisho, desturi na elimu, hivyo upoteaji wa nyenzo za watanzania za kushirikisha sanaa zao duniani


TAASISI YA UUNGANISHAJI WA PENGO (BRIDGING THE GAPS)
Taasisi ya Uunganishaji wa Pengo (Bridging The Gaps – BTG Inc.) ni taasisi isiyo ya kiserikali, isiyopata faida, yenye kuongozwa na vijana mjini Quezon-Ufilipino. Taasisi hii inayainisha jukumu linalopaswa kutekelezwa na vijana katika kusaidia jamii zisizojiweza, huku ikijisaidia yenyewe kukua kwenye mchakato kama kifaa kinachowajibika na kujihusisha zaidi katika jamii za kitaifa na kimataifa, kwa kutumia ujuzi wake, ufahamu, na uwakili kwenye nguzo kuu nne za taasisi ambazo ni (1) elimu, (2) maendeleo endelevu, (3) huduma ndogo ndogo za kifedha na ujasiriamali, pamoja na (4) tamaduni na urithi. Hatimaye, ufanyaji kazi kwa kujitolea, ujengaji mitandao yakinifu, na ushiriki wa vijana umeendelea kushikiliwa kama kanuni kuu ambazo taasisi zinasimamia, ikijiwezesha kuweka chachu ya ukuaji chanya wa kijamii ndani ya ajenda zake.
MTANDAO WA UBADILISHAJI TAMADUNI KWA VIJANA TANZANIA
Mtandao wa ubadilishaji tamaduni kwa vijana Tanzania ni taasisi ya kimaendeleo inayoongozwa na vijana iliyopo Dar es Salaam-Tanzania. Misheni yao ni kuwashirikisha vijana kwenye miradi ya kijamii nchini na nje ya nchi, iliyojikita katika elimu, maswala ya kijinsia, afya, tamaduni, ujana na utunzaji wa mazingira pamoja na maendeleo endelevu. Mtandao wa ubadilishaji tamaduni kwa vijana Tanzania (TYCEN) unasaidia uunganishaji wa vijana kwenye jamii, na kutia moyo harakati zao katika maisha ya kijamii, desturi na kiuchumi kwa ajili ya jamii zao ndani na nje ya mikoa yao, ikiwa ni pamoja na kutengeneza tabia na ujuzi wa ushiriki hai wa kiraia. Shughuli zake zinajumuisha na kunufaisha makundi yasiyo rasmi ya vijana wenye umri kati ya 15-35 kutoka pande zote za nchi.

WOMEN EMPOWERMENT THROUGH SPORTS PARTNER ORGANIZATIONS
