Kozi ya Mafunzo ya “Riadha – nguvu ya kuwezesha wanawake” ilianzishwa nchini Kenya na taasisi ya kijamii ya Neema mnamo Mei 2018. Mafunzo yalihusisha wafanyakazi vijana 24 na viongozi vijana ambao walipewa mafunzo na zana za kufanya kazi na vijana wasiojiweza katika sehemu fukara mijini na vijijini, wakiwa na vyombo toshelezi, mbinu na ujuzi wa jinsi ya kutumia nyenzo hizi kutoa elimu kupitia michezo. Kisha nao wanakua wachochezi wa uwezeshaji wa wanawake kwenye mitaa yao.
Washiriki wote walipata nafasi mashuhuri ya kuendeleza ufahamu na ujuzi wao pamoja na kuboresha ubora wa kazi katika taasisi zao. Shughuli mbalimbali ambazo programu ya mafunzo haya ilizifanya ni pamoja na uwezeshaji wa kufikia malengo. Malengo ya kozi ya mafunzo haya yalikua:
- Kujadili hali ya wasichana na wanawake waliopo Ulaya, Asia, na Afrika, katika swala la uhusishaji jamii.
- Kushirikisha mienendo mizuri inayohusisha usawa wa kijinsia
- Kupambana na mitazamo potofu inayohusu nafasi ya mwanamke kwenye jamii
- Kuelewa sababu za kutokua na usawa wa kijinsia pamoja na matokeo yanayotokana na hili
- Kuelewa kanuni za elimu kupitia nyenzo ya riadha
- Kutengeneza njia mpya za kuwezesha wanawake kwa kutumia vifaa vya michezo
- Kuwawezesha wanawake katika swala la uhusishwaji katika jamii
Mwanzoni mwa kozi hii ya mafunzo, kila mwakilishi alishirikisha washiriki wote kazi zinazofanywa na taasisi yake pamoja na kuwasilisha programu zao za kuwawezesha wanawake, ili kumwezesha kila mmoja kupata uelewa yakinifu wa mada na njia mbalimbali zinazotumika. Kisha, washiriki walijadili njia hizo mbalimbali na mikakati ya kukabiliana na mitazamo potofu inayohusu nafasi ya mwanamke kwenye jamii. Washiriki wote wa kozi hii ya mafunzo walinufaika pia kutoka kwenye matembezi mbalimbali: – Mtaa wa mabanda wa Mathare Nairobi, ambapo washiriki walitembelea kanisa la sehemu hiyo, Ofisi ya taasisi ya Jamii ya Neema na shule katika jamii hiyo, ambapo washiriki walijipatia uelewa mpana juu ya utekelezaji wa elimu nchini Kenya, pamoja na mfumo wa kazi wa taasisi ya kijamii ya Neema na jinsi wanavyokabiliana na tatizo la ubaguzi wa kijinsia.
Kupitia matembezi haya, washiriki walijadili hali ya wasichana na wanawake waliopo Ulaya, Asia, na Afrika, na wakaelewa sababu za ubaguzi wa kijinsia pamoja na matokeo yanatokana na hilo. – Mathare Youth Sports Association (MYSA), where participants learnt about the various ways that the Association uses sports to engender broad socio-economic development, while also effecting positive social change.
Representatives of MYSA presented their work system, their key achievements and put a special accent on their programs for women empowerment. Through the visit, the participants of the Training Course received good practices related to ensuring gender equality and understood the principles of Education through Sport methodology and generated new women empowerment through sport tools.