KUHUSU MRADI
Uwezeshaji Wanawake Kupitia Riadha
Ubaguzi wa kijinsia na upotevu wa usawa ni swala la kimfumo lililosambaa na linalojulikana vema ndani ya Ulaya na Duniani. Katika hali halisi za kitamaduni na kitaifa, utengenezaji wa usawa imara wa kijinsia unayumbishwa na vikwazo sugu pamoja na ubaguzi dhidi ya mabinti. Vikwazo vilivyotajwa vinahusisha asili ya vitu (kama kushindwa kufikia soko la kazi, mishahara midogo kwa kulinganisha na ile wanayopewa wanaume, uwepo hafifu wa wanawake kwenye nafasi za juu za biashara na kwenye sekta za umma) na zinazohusiana na mizunguko ya kijamii ambayo uwezo wa kupenya wa mitazamo hii unapelekea kwa namna moja ama nyingine, mitazamo potofu na ushirikina unaowazuia mabinti kujitengenezea majukumu.

JIFUNZE ZAIDI
“Uwezeshaji Wanawake kupitia Ridhaa” (WEtS) ni ujengaji uwezo katika uwanja wa mradi wa vijana, wa muda wa miezi 24, ambao unahusisha taasisi 6 kutoka bara la Ulaya (Bulgaria na Italy), Afrika (Kenya na Tanzania) na Asia (Nepali na Ufilipino). Mradi huu unatupa nafasi ya kuendeleza, kujaribu na kusambaza mbinu mpya za elimu kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake kupitia ridhaa kwa lengo la kuboresha uwezo wa taasisi shirikishi na zaidi.
MADHUMUNI YA UWEZESHAJI WANAWAKE KUPITIA RIADHA
- Kushirikisha, kuhamisha, kuboresha na kutengeneza zana na mienendo kwa ajili ya uwezeshaji wa mabinti kupitia ridhaa.
- Kuwafunza wafanyakazi vijana na viongozi kuhusu elimu isiyo rasmi na jinsi ya kutumia riadha kuwezesha wanawake mabinti.
- Kutengeneza ukurasa wa tovuti, ambao utatumika kama nyanja ya mawasiliano kwa washiriki wote hata baada ya mradi kuisha.
- Kutengeneza mtandao wa kimataifa endelevu na wa muda mrefu wa taasisi zinazofanya kazi ya kuwawezesha mabinti kupitia ridhaa.
- Kutafiti juu ya hali ya programu za kuwawezesha mabinti katika nchi zinazohusika na kufanya utafiti wa ujumla wa nchi zote zilizojumuishwa.
- Kuleta mabadiliko ya kijamii kupitia shughuli za kuongeza uelewa na matukio ya riadha “Uwezeshaji Wanawake kupitia Riadha” katika ngazi za kitaifa kwenye nchi,mikoa husika na katika ngazi ya dunia.

Ubaguzi, mitazamo potofu na ukatili dhidi ya wanawake upo miongoni mwa nchi shirikishi na hususani katika zile zilizotengwa na zenye maendeleo hafifu. Sifa za ukoo zinazotofautisha mahusiano ya kifamilia na mfumo wa jamii katika nchi zilizohusishwa, zikijumuishwa na mitazamo ya kihafidhina katika ngazi ya jamii, hutenda kazi kama dereva wa jamii anayeidhinisha ishara za ubaguzi, mitazamo potofu na ukatili ambayo ina hatari ya kusafirishwa kwenda vizazi vichanga.
Wakati huo huo, athari ya hisia na saikolojia ya ubaguzi uliounganishwa kwa kutengwa kwa jamii unatumia hali ya upotevu wa usalama na ukulifu unaosababisha mabinti kujitoa katika kushiriki mambo ya kijamii na kiuchumi, kitu ambacho kitaleta tofauti kubwa katika kufikia malengo yao binafsi na kutengeneza mabadiliko yenye chanya katika jamii zao.
Chama Shirikishi kinajumuisha asasi za vijana zilizoazimia kufikia fremu ya kanuni ya usawa wa kijinsia, na zilizo na uzoefu katika utumiaji elimu kwenye riadha. Taasisi zote shirikishi zinafanya kazi katika maeneo ya vijijini kwa ajili ya kufikia malengo yaliyojikita kwenye jamii kupitia riadha na nyenzo zisizo rasmi za elimu, na pia zina uhusiano wa moja kwa moja na malengo ya vijana kwenye jamii. Wao wanafanya kazi kama wakuzaji wa uwezeshaji wa wanawake, hususani wanawake wenye nafasi hafifu, wanawake waliotelekezwa, wanawake wasioweza kufikia mafunzo ya kujiendeleza, wanawake waliotengwa. Mradi huu wa sasa ulitengenezwa kutoka kwenye mazingatio yaliyoshirikishwa yaliyohusu changamoto inayowekwa na mapengo sugu ya kijinsia, kutokuwepo usawa na mitazamo potofu iliyopo kwenye nchi zote shirikishi za chama.

Ili kufikia malengo, taasisi sita kutoka nchi sita za mabara matatu zitatoa jumla ya matukio sita ndani ya kipindi cha mzunguko wa mradi katika maeneo ya jeografia tofauti:
- “Mkutano wa uzinduzi nchini Italia mnamo Machi 2018, ukiwa na viongozi 3 kwenye kila taasisi
- Kozi ya mafunzo nchini Kenya mnamo Mei 2018, ikiwa na viongozi/wafanyakazi vijana 4 kwenye kila taasisi
- Kivuli Kazi nchini Ufilipino mnamo Agosti 2018, ukiwa na viongozi/wafanyakazi vijana 2 kwenye kila taasisi
- Mkutano wa viongozi nchini Nepali mnamo Novemba 2018 ukiwa na viongozi/wafanyakazi vijana 3 kwenye kila taasisi
- Mabadilishano ya vijana nchini Tanzania mnamo January 2019, yakiwa na vijana wasiojiweza 6 kwenye kila taasisi
- Mkutano wa hitimisho nchini Bulgaria mnamo Mei 2019, ukiwa na viongozi/meneja wa miradi 3 kwenye kila taasisi
“Uwezeshaji Wanawake kupitia Riadha” umekusudiwa kuwa na athari ya muda mrefu kwa wadau wanaohusika, katika ngazi binafsi, ngazi ya taasisi na kwenye ngazi ya mfumo kiujumla. Athari itadumu zaidi ya kipindi cha mradi, na kugusa zaidi ya taasisi zilizohusika.”
SAFIRI NASI

VIAINISHI VYENYE KUKADIRIKA:
- Matukio 6 yamefanywa ndani ya nchi 6
- Mitaala ya kitaifa iliyotekelezwa katika kila nchi husika na mtaala mmoja wa ujumla
- Matokeo ya mwisho – ukurasa wa mtandao; kitabu chenye desturi nzuri, nyenzo salihi, mtaala wa kitaifa na kiujumla; video
- Kila nchi inaratibisha kampeni mbili za kuchochea uelewa pamoja na Hafla ya Kiriadha “Uwezeshaji wanawake kupitia riadha“
- Namba ya machapisho na makala za mradi katika vyombo tofauti vya habari