Kikao cha viongozi wa kimataifa Nepali pamoja na taasisi enyeji “Go Sports Nepal” mnamo Oktoba 2018 kilijumuisha viongozi 15 ambao walifanya tathmini ya mradi katika kipindi cha kati. Washiriki walijadili matukio ya jamii yaliyohusisha mradi katika kila nchi shiriki.
Tumetembelea uwanja wa mpira wa miguu uliopo kwenye shule ya serikali ya Nepalya, ambapo “Go Sports Nepal” iliratibisha shughuli ya kukuza uelewa kwa wachezaji wa mpira wa miguu wa kike 60. Siku ya pili ya mkutano, tulikuwa na mkutano na Bwana David Durkan, ambaye anaratibisha shughuli za kijamii zinazohusisha wanawake wa milimani kutoka Nepali na anayefanya kazi moja kwa moja na taasisi ya wanawake ya sanaa ya Beni handi.
Pia, tumepata furaha ya kutembelea Jumuiya ya mpira wa miguu ya Nepali (ANFA) iliyopo Satdobato, ambapo afisa wa mahusiano ya kimataifa Bwana Nabin Pandey ametuwasilishia programu za jamii walizonazo kwa ajili ya mabinti na kutushirikisha changamoto wanazopitia huko Nepali katika kufikia ngazi za kitaifa, kuwaweka, pamoja na kuhusisha wanawake kwenye shughuli za kimichezo za mara kwa mara.