Leo tuna furaha kubwa kuzindua mradi wa Uwezeshaji Wanawake Kupitia Riadha nchini Sardinia (Italia). Tukiwa pamoja na viongozi wa Banda la Mabingwa, Asasi ya Mine Vaganti, Shirika la Kijamii la Neema, BTG.Philippines, Go Sports Nepali na Mtandao wa Vijana wa Kubadili Tamaduni Tanzania, tumekusanyika Italia kukutana kwa pamoja kwa mara ya kwanza na kujadili vipengele vyote vya maudhui ya shughuli 5 zijazo zilizopo kwenye mradi huu!
Na ipi ni siku bora ya kuanza mradi huu wa uwezeshaji wanawake zaidi ya tarehe 8 Machi – Siku ya Wanawake Duniani 🙂