Kikao cha uzinduzi kilichofanyika Italia pamoja na taasisi ya Mine Vaganti mnamo Machi 2018. Kwenye kikao tulitengeneza fremu ya ushirikiano, tukatengeneza mpango wa utekelezaji, mpango wa mahusiano, mpango wa usambazaji, mpngo wa fedha, tukapangilia utengenezaji wa chapa ya ya mradi na ukurasa wa Facebook.
Tulipanga kwa undani hatua za kuchukua. Tulitembelea shule ya elimu ya ufundi na mafunzo ya michezo ya “Pitagora” . Katika siku ya pili ya mwiho ya kikao cha uzinduzi, kulikua na tukio na hadhara mjini Corsa, Rosa ambapo wanariadha maarufu pamoja na makocha mashuhuri kutoka mkoa wa Sardinia walitoa hotuba kuhusu thamani ya michezo na umuhimu wa wanawake. Bwana Didar Amin, Bi Arunima Dahal, Bibi Khammela Gragas na Bi Shirin Amin walipanda jukwaani na kuwasilisha mradi, nafasi zake na athari zake na ni kwa jinsi gani taasisi za nje zinaweza kufikia matokeo yake na kuwa mabalozi wa mradi wa “Uwezeshaji wa Wanawake kupitia riadha”.
Jumla ya watu waliofikiwa walikua ni zaidi ya 300, hivyo iliwabidi viongozi wa mradi wakutane na wanufaika uso kwa uso katika mkoa wa Sardinia. Shughuli hii ilitathminiwa na kuripotiwa kufikia watu zaidi ya 1000 kutoka Sardini yote. Katika kipindi cha kikao cha uzinduzi, Bi Arunima Dahal (kijana kiongozi na mfunzi wa GoSportsNepal) alikaribishwa na klabu kubwa ya wanawake ya Sardinia (S.E.F. Torres 1903), ambapo alikwenda na mkurugenzi wa GoSportsNepal na wameweza: (1) kuwasilisha mradi kwa meneja na kocha wa klabu na (2) kuwasilisha mradi kwa wachezaji wa mpira wa miguu wasichana 30 wa klabu hiyo, pamoja na kuwasilisha nafasi zake katikamchezo wa mpira wa miguu ambao Arunima ulichukua.