Jukwaa la Uhitimisho la “Uwezeshaji Wanawake Kupitia Riadha” lilifanyika Tanzania mwezi wa tano 2019 na lilijumuisha wafanyakazi vijana 18 pamoja na wafanyakazi waliokusanya matokeo yote ya mradi, na kukamilisha kitabu cha mienendo bora, wakahakikisha uonekanaji wa mradi katika taasisi shirikishi pamoja na nchi elekezi, wakafanya mapitio na ripoti ya mwisho ya mpango wote wa fedha na utawala, wakapanga namna fanisi ya ufuatiliaji wa mradi pamoja na kupanga mikakati mipya na washiriki wapya.
Katika Jukwaa la Uhitimisho, kila taasisi imewasilisha shughuli zake na mafanikio yake katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huu. Wakilishi zaidi ya 130 kutoka taasisi zifuatazo walikuwepo:
1. Fountain Gate Academy
2. Baobab Girls Secondary School.
3. Roots & Shoots Tanzania.
4. St. Mary’s Secondary School.
5. JrNBA Tanzania Office.
6. Tabasamu Consultant.
7. Dept. Of Creative Arts – Univ. Of Dar es salaam.
8. CHAMWINO ARTS CENTER TANZANIA


