Katika kikao cha uzinduzi wa mradi wa “Uwezeshaji Wanawake Kupitia Riadha” nchini Sardinia (Italia), Árü Ñeéma Dàhãl amepata nafasi ya kipekee ya kukutana na viongozi wa klabu bingwa ya mpira iliyopo Sassari – FC Sassari Torres Femminile na kuweza kushiriki mchezo mmoja na timu hiyo ya wanawake! Hili pia lilikua zao la ushirikiano mzuri uliopo kati ya meneja wa klabu pamoja na kiongozi wa taasisi ya vijana na michezo “GoSportsNepal” – Bwana Sunil Shrestha, ambaye alishirikisha desturi nzuri na vifaa vya kuwawezesha mabinti kupitia mchezo wa mpira wa miguu!